Mshambuliaji wa Yanga Lazarus Kambole ambaye anaitumikia Zesco United kwa mkopo, amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia (wachezaji wa ndani) ambacho kitafanyiwa mchujo kabla ya kuungana na nyota wanaocheza nje ya nchi
Kambole amekuwa na kiwango bora katika ligi kuu ya Zambia akipachika mabao manne tangu alipojiunga na Zesco mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huuΒ
Kocha Mkuu wa Zambia Avan Grant anatarajiwa kumjumuisha kwenye kikosi chake cha mwisho kuelekea mechi za kuwania kufuzu Afcon 2023
Kambole huenda akakutana na mshambuliaji mwingine wa Yanga Kennedy Musonda ambaye ni miongoni mwa wachezaji walioitwa ambao wanasakata kabumbu nje ya Zambia

ADVERTISE HERE