Kwa Mudathir Nabi aliahidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Mar 2023
Kwa Mudathir Nabi aliahidi

Wakati Yanga ilipomtangaza Mudathir Yahya kama usajili wa kwanza kwenye dirisha dogo wapo mashabiki waliponda usajili huo eti kwa kuwa hakuwa akitoka nje ya nchi

Imekuwa ni kasumba kwa mashabiki wa soka nchini kupenda zaidi usajili wa wachezaji kutoka nje ya nchi katika dirisha la usajili kuliko wale wa ndani

Mudathir tayari anewathibitishia Wananchi kuwa ni ingizo bora sana kwenye kikosi cha Yanga

Usajili wake haukuzuka tu, lilikuwa pendekezo la kocha Nasreddine Nabi ambaye alihitaji kuziba nafasi ya Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye alijiengua kikosini

Wakati anasajiliwa ilikuwa haionekani Mudathir anawezaje kuwa mbadala wa Feisal?. Nabi alisema Mudathir atakapoiva atakuwa mchezaji wa kutegemewa kwenye kikosi cha kwanza

Mudathir amedhihirisha hilo mapema kwani kwa sasa sio rahisi tena kwa Nabi kumuweka nje

Uwezo wake wa kucheza zaidi ya nafasi moja kwa ufasaha uwanjani unamfanya kuwa mchezaji wa aina yake

Katika mchezo uliopita dhidi ya Real Bamako, Mudathir alianza eneo la kiungo cha chini akiwa sambamba na Yannick Bangala na juu yao akiwa Stephane Aziz Ki

Lakini baada ya dakika 45, Nabi akalazimika kumtoa Aziz Ki kumuingiza Khalid Aucho na Mudathir kusogea juu

Ndio wakati ambao Yanga ilitawala mchezo na kufanya eneo la kiungo litulie. Muda ana faida akiwa na mpira na hata asipokuwa na mpira

Ni mchezaji asiyetabirika anapiga pasi katika maeneo mazuri wakati timu inaposhambulia na bila mpira Muda ni mchezaji asiyechoka, anakimbia sana uwanjani na mahiri kwenye kupora na kuirejesha mipira kwenye himaya ya Yanga

Nabi amedhihirisha kwa mara nyingine yeye ni Profesa wa soka! Wale wachezaji wanao-onekana wa kawaida katika timu nyingine, wanakuwa bora katika timu yake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’