Wananchi kutoka mikoani kuifuata Monastir Dar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Mar 2023
Wananchi kutoka mikoani kuifuata Monastir Dar

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wanawasiliana na Matawi ya klabu ya Yanga mikoani kuandaa utaratibu wa kusafiri kuja jijini Dar es salaam kushuhudia mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir ambao utapigwa Jumapili March 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Kamwe amesema wanatarajia kuwa na Mashabiki wengi kutoka mikoani hivyo amewataka Mashabiki wa jijini Dar es salaam 'wasilale' ili kuhakikisha Jumapili uwanja wa Benjamin Mkapa unajaa

"Tunawasiliana na Matawi ya Yanga mikoani ili kuweka sawa taratibu za safari za mashabiki kutoka mikoani wanaokuja kushuhudia mchezo dhidi ya US Monastir. Tunawaomba na wale wa jijini Dar es salaam msilale, mechi hii ni kubwa tuhakikishe tunaujaza uwanja wa Mkapa kuwahamasisha wachezaji wetu waweze kushinda siku ya Jumapili," alisema Kamwe

"Monastir tuna deni nao, na lazima tulipane. Sijui Monastir ametufungaje kule kwao. Pamoja na kutaka kufuzu lakini lazima deni lilipwe. Tunakwenda na FullHouse Full Shangwe waje tumalizane nao kwa Mkapa," alisema Kamwe

Kamwe ametangaza viingilio vya mchezo huo ni VIP A Tsh 30,000/-, VIP B Tsh 20,000/-, VIP C Tsh 10,000/- na Mzunguuko Tsh 3,000/-

Tiketi tayari zimeanza kuuzwa kwenye mifumo ya ununuzi wa tiketi kwa njia ya simu na Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani

Kamwe ametangaza kauli mbiu kuelekea mchezo huo ni FULL HOUSE, FULL SHANGWE WAJE TUMALIZANE...!

Yanga itafanya tukio kubwa la Hamasa siku ya Jumatano, Manzese jijini Dar es salaam ambapo Wananchi watapata nafasi ya kununua tiketi na kupata burudani kutoka kwa Wasanii mbalimbali

Siku ya Ijumaa Yanga itaendesha zoezi la kuchangia damu Hospitali ya Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es salaam

Siku ya Jumamosi, utaratibu wa 'jogging' kwa Wanachama na Mashabiki utaendelea kama walivyofanya katika mechi zilizopita

Siku ya Jumapili ambapo mchezo utapigwa saa 1 usiku, kuanzia saa 9 mchana kutakuwa na parade la robo fainali ambapo Wananchi wataandamana kutoka Jangwani kuelekea uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’