Kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir ambao utapigwa Jumapili, March 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, klabu ya Yanga imeandaa zoezi kubwa la uchangiaji damu kwa ajili ya Hospitali ya Mloganzila
Zoezi hilo litafanyika kuanzia Ijumaa asubuhi Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani na Hospitali ya Mloganzila
Kwa wale ambao watashiriki zoezi hilo, watapata tiketi bure kushuhudia mchezo dhidi ya US Monastir ambao Yanga inahitaji kushinda ili kutinga robo fainali
Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji ametoa tiketi 1000 kwa wote watakaojitokeza kwenye zoezi hilo siku ya Ijumaa
Aidha, Yanga imekaribisha Makampuni/Taasisi kununua tiketi kwa ajili ya kuwazawadia mashujaa wote watakaojitolea damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wengine
