Eymael ashangaa uzushi dhidi ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Mar 2023
Eymael ashangaa uzushi dhidi ya Yanga

Kocha wa zamani wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa timu hiyo haijafungiwa kusajili madirisha matatu na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kwa kosa la kuchelewa kumlipa madai yake kama ilivyoripotiwa na chombo kimoja cha habari mapema leo

Eymael amebainisha kuwa uamuzi uliotolewa na FIFA ni kuitaka Yanga kulipa madai yake ili isikumbane na adhabu hiyo.

Kauli hiyo ya Eymael imekuja muda mfupi baada ya mtandao mmoja wa Afrika Kusini kudai kuwa Yanga imefungiwa kusajili kwa madirisha matatu kwa kosa la kutomlipa kocha huyo.

"Nadhani walioandika taarifa hiyo wameripoti kinyume. FIFA walitoa uamuzi na pande zote tumejulishwa kwamba Yanga wanatakiwa kunilipa stahiki zangu ndani ya siku 45 na iwapo wakishindwa kufanya hivyo, kuna adhabu kubwa zaidi watapewa ikiwemo ya kufungiwa kusajili," alisema

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema taarifa hii imeibuliwa kwa nia ovu ya kuwavuruga mashabiki na wanachama wa Yanga kuelekea mchezo dhidi ya US Monastri ambao utapigwa Jumapili

Kamwe amesema suala la Eymael na Yanga sio geni na pande zote zimekuwa na mawasiliano Yanga ikiwa tayari imeshalipa sehemu ya deni hilo

"Kwa jinsi taarifa hii ilivyoripotiwa utaona hakuna nia njema kwa Yanga, lilikuwa ni suala la kufanya utafiti kidogo tu kijiridhisha na ukweli wa taarifa hiyo kabla ya kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii"

"Imekuwa kawaida kila Yanga inapoelekea kwenye mchezo muhimu kuna jambo linatokea ili kutuondoa kwenye reli lakini sisi tunasema wameshindwa. Focus yetu ni mchezo dhidi ya Monastir," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’