Kikosi cha US Monastir kimewasili nchini Alfajiri ya leo Ijumaa kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga
Mtanange huo utapigwa Jumapili, March 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 1 usiku
Mechi muhimu kwa Yanga kuibuka na ushindi ili kutinga robo fainali ya michuano hiyo
Mkufunzi wa timu hiyo Darco Novic amesema wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wao hawana presha kwa kuwa tayari wamejihakikishia tiketi ya robo fainali
Novic amesema itakuwa mara ya kwanza wachezaji wake kucheza katika uwanja ulifurika mashabiki hivyo anaamini mchezo utakuwa mzuri
ADVERTISE HERE