Full House Full Shangwe imelipa - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Mar 2023
Full House Full Shangwe imelipa - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amewapongeza mashabiki waliojitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa jana katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir

Licha ya mvua, Wananchi walijitokeza kwa wingi uwanjani na zaidi ni vile walivyojitolea na kuwa sehemu ya ushindi wa mabao 2-0 ambao uliwapeleka Wananchi robo fainali huku wakiongoza kundi D

Arafat amesema walichokishuhudia wapinzani uwanjani wa Benjamin Mkapa lazima kiwatishe na huu ni mwanzo tu wa mafanikio makubwa yanayokuja

"Nani atauzima moto huu wa Yanga? Nani haogopi mziki huu wa Wananchi? Nani anaweza kuthubutu kufikiri atatoka salama kwa Mkapa?"

"Hatimae FULL HOUSE FULL SHANGWE imelipa tena kibabe mpaka wanaogopa, hakika tuna kila sababu ya kumshukuru Mola wetu kwa kutufikisha hatua hii kubwa. Yanga tumethibitisha kwamba maneno kwetu kidogo mpira mwingi tukitinga kibabe Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika"

"Hii leo haikuwa tu kufuzu kama wale wenzetu lakini tunaongoza kundi letu tukiwashusha Us Monastir kwa kufikisha alama 10 lakini tukiwa na tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa"

"Tunafuzu Leo tukiwa hatujaangusha pointi yoyote nyumbani.Wananchi Wananchi Wananchi Wananchi Wananchi Wananchi nasemajeee HAKUNA ALIYETOKA SALAMA KWA MKAPA nani anaweza? Wananchi hii leo mmeithibitishia Afrika ninyi ndio mashabiki na wanachama wenye hamasa na ari kwa timu yenu, bila kujali mvua kubwa iliyokuja leo lakini mkasema hii ni baraka bado mkafanya kweli kwa kuitikia wito wa kuja kuifurisha Mkapa Stadium"

"Nyie ni watu bora sana,mmetuheshimisha tunasema AHSANTENI Sasa niwape mchongo Wananchi pigeni bata na kutamba kwa ubora wa timu yenu lakini tunakwenda kuweka historia kwa kushinda ugenini lakini kubwa tunataka kuongoza makundi ili kujitofautisha na wote"

"Tambeni na jivunieni kuipenda klabu bora kama hii, imeisha hiyoooo," aliandika Arafat kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
28m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
46m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
52m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’