Yanga yamtisha kocha US Monastir

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Mar 2023
Yanga yamtisha kocha US Monastir

Jumapili ya wiki iliyopita Yanga iliandika historia ya kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi US Monastir ya Tunisia

Ulikuwa ushindi ambao sio tu uliipeleka Yanga robo fainali, bali pia uliwahakikishia Wananchi kukaa kileleni mwa kundi D wakifikisha alama 10 sawa na Monastir lakini Yanga ikiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa

Baada ya kipigo, kocha mkuu wa US Monastir Darko Novic alikubali kuwa amepoteza mchezo dhidi ya timu bora huku akiwatabiria Wananchi kuwa wanaweza kutinga nusu fainali

US Monastir ni moja ya timu bora sana msimu huu, kikosi chao kina thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 20 wakiwa na msimu mzuri katika ligi ya Tunisia

Walifuzu play-off katika ligi ya kwao wakiwa vinara wa kundi B na sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye play-off wakiwa na alama saba sawa na Esperance inayoshika nafasi ya pili

Etoile Du Sahel inaongoza ikiwa na alama 9 lakini imecheza mechi moja zaidi ya Monastir na Esperance

Mfumo wa ligi kuu ya Tunisia huchezwa katika makundi mawili ambapo timu nne za juu kwenye kila kundi zinafuzu kucheza ligi ya play-off ambayo hutoa bingwa

Lakini kocha wao Novic amekiri kushangazwa na uwezo wa Yanga walioonyesha katika dimba la Mkapa katika mchezo ambao Monastir walipiga shuti moja tu lililolrnga lango

"Kwangu mimi nawaona Yanga watafika mbali kwa kuangalia ubora wa timu yao na kuwa na kocha mzuri (Nabi) ambaye anafahamu vyema mashindano haya"

"Nabi ameiweka Yanga mahali salama kimbinu na kwamba hata timu yake inapokuwa nyuma inacheza vizuri," Novic alinukuliwa na Mwanaspoti

"Tulipocheza nao tukashinda (2-0) muda wote hatukuwa na utulivu wa kuona kama tumemaliza mechi. Nawaheshimu kwa kuwa wanaonesha kuna kazi kubwa kocha wao amefanya. Nilipokuwa nawafuatilia na kuangalia mechi zao sikuona kama kuna mchezo wamezidiwa umiliki wa mpira"

"Napenda wanavyocheza, wanakulazimisha, wakati wote wanataka mpira uwe katika miliki yao. Tulipocheza nao kisha kucheza na Tp Mazembe tuliona tofauti kubwa ilitosha kuona kwamba Yanga watakuwa washindani wetu wakubwa katika kundi letu"

"Silaha ya pili ya Yanga ni wale washambuliaji wawili kwenye eneo la mbele, yule namba 9 (Mayele) ni hatari anajua sana kufunga lakini pia anakasi. Kuna yule jezi namba 25 (Musonda) ndio tatizo zaidi, unapokuwa na washambuliaji wa namna ile wanawalazimisha mabeki kupoteza nidhamu yao kutokana na kasi yao. Kitu kibaya zaidi wanacheza kwa ushirikiano mkubwa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’