Mzize anaandaliwa kuiadhibu TP Mazembe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Mar 2023
Mzize anaandaliwa kuiadhibu TP Mazembe

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anamuandaa mshambuliaji kinda Clement Mzize kuwakabili TP Mazembe kwenye mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika

Mchezo huo utapigwa Jumapili, April 02 saa 10 jioni huko Lubumbashi, DR Congo Yanga ikihitaji ushindi ili kuwa na uhakika wa kumaliza kinara wa kundi

Mzize ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao hawakuitwa katika timu za Taifa akiendelea kujifua na wenzake Avic Town timu ikiwa imeingia kambini jana

Takribani wachezaji 12 wa Yanga wako kwenye majukumu ya timu za Taifa ikiwa ni pamoja na washambuliaji tegemeo Fiston Mayele na Kennedy Musonda

Wakati Yanga ikitarajiwa kuondoka nchini Alhamisi kulekea DR Congo, baadhi ya nyota wanaocheza nje ya nchi wao wataungana na timu hukohuko Congo

Mzize tayari amethibitisha yuko tayari kwa majukumu makubwa kwenye kikosi cha Yanga msimu huu akiwa amepachika mabao 10 katika mashindano yote

Nabi amemtumia Mzize katika mechi zote tano za hatua ya makundi, akimpa dakika 10 za mwisho

Bado hajafanikiwa kufunga lakini ni mchezaji mwenye kiu ya kupachika bao katika michuano hiyo na kuingia katika vitabu vya kumbukumbu vya klabu ya Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’