Droo ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kombe la Shirikisho, itafanyika leo Jumatano April 05 huko Cairo, Misri
Wananchi Yanga watakuwa miongoni mwa timu nane ambazo zitahusika katika droo ya robo fainali ya kombe la Shirikisho
Yanga ikiwa kinara wa kundi D, itapangwa katika poti moja na vinara wa makundi mengine A,B na C ambao ni Malumo Galants, Asec Mimosas na AS FAR
Yanga itapangwa na timu zilizomaliza katika nafasi ya pili isipokuwa US Monastir ambayo imeshika nafasi ya pili katika kundi lililoongozwa na Yanga
Timu zilizomaliza nafasi ya pili katika makundi mengine ambazo moja inaweza kupangwa na Yanga ni USM Alger, Pyramids na Rivers United
Droo itafanyika saa 3:30 usiku kwa saa za Tanzania
ADVERTISE HERE