Kikosi cha Yanga kesho Jumanne kinashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Township Rollers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika, raundi ya kwanza.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema tayari amekiandaa kikosi chake kikamilifu kuhakikisha wanashinda mchezo huo unaopigwa nyumbani.
“Maandalizi yameshakamilika muda mrefu, ukiwa na mtihani huwezi kujiandaa kwa siku moja kabla au wiki, nilishakiandaa kikosi changu muda, tunatakiwa tushinde ili tusonge mbele. Tunawahehimu wapinzani wetu, lakini tunataka ushindi nyumbani,†amefunguka Lwandamina.
Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kesho ikiwa kwenye kiwango bora baada ya kucheza michezo tisa bila kupoteza. Katika hiyo michezo, imeshinda michezo sita mfululizo ya ligi kuu ya Vodacom.
Yanga imedhamiria kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kabisa barani Afrika. Kampeni hiyo ni lazima ianze na ushindi mnono nyumbani ili kurahisisha kazi katika mchezo wa marudiano utakaopigwa March 17 nchini Botswana.

ADVERTISE HERE