Mendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine atahudhuria droo ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika sambamba na Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika leo Jumatano
Mtine aliondoka nchini jana jioni tayari kwa hafla hiyo itakayofanyika jijini Cairo kuanzia saa 3:30 usiku
Yanga ni moja kati ya timu nane zitakazosubiri kujua watakutana na timu ipi kwenye hatua ya robo fainal kwa upande wa shirikisho.
Yanga imefuzu hatua ya robo fainali baada ya kuongoza kundi D. Timu tatu ambazo moja inaweza kungukia kwa Yanga ni USM Alger (Algeria), Pyramids (Misri) na Rivers United (Nigeria)
Mechi ya kwanza itapigwa ugenini na mechi ya pili kupigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mechi zote mbili zitapigwa kati ya April 22-30 2023
ADVERTISE HERE
Yanga SC Stories