Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema mechi ya leo ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ina umuhimu wa kipekee katika mpango wao wa kutwaa ubingwa wa pili mfululizo
Majira ya saa 1 usiku Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili Kagera Sugar katika mchezo ambao matokeo ya ushindi yatazidi kuisogeza Yanga karibu na ubingwa
Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa winga uwanja wa Azam Complex kuishangilia timu yao ili kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu
"Leo tuna mechi muhimu sana dhidi ya Kagera Sugar, nawaomba mashabiki wa Yanga mje kwa wingi dimba la Azam Complex kuhakikisha tunaipa sapoti timu yetu ili tushinde mchezo huu"
"Tunafahamu Kagera Sugar ni wasumbufu lakini sisi tumejipanga kwa ajili ya ushindi ili tufanikishe malengo yetu. Tukishinda mchezo huu halafu tukashinda Kariakoo Dabi siku ya Jumapili, tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa"
"Tunahitaji kwenda Nigeria kukabiliana na Rivers United katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika tukiwa tayari tumeweka sawa hesabu zetu za ubingwa wa Ligi Kuu," alisema Kamwe
Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikikusanya alama 65 baada ya mechi 24 wakiwa mbele kwa alama tano dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 60 wakiwa wamecheza mechi 25
