Mwamnyeto afunguka wanavyokabiliana na ratiba ngumu mwezi April

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Apr 2023
Mwamnyeto afunguka wanavyokabiliana na ratiba ngumu mwezi April

Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema Aprili ni mwezi mgumu kwao kutokana na mitego ya mechi wanazokabiliana nazo, lakini uwepo wa Helmy Gueldich raia wa Tunisia amewalainisha mambo.

Ndani ya mwezi huu, wamekutana na Geita Gold mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kushinda wametinga nusu fainali ambapo watakutana na Singida Big Stars

Ukiachana na hilo, mechi za Ligi Kuu wanakutana tena na Kagera Sugar leo, mchezo wanaohitaji kushinda ili kuendelea kuusogelea ubingwa maana wanahitaji pointi 11 ili ifikishe pointi 76 ambazo haziwezi kufikiwa na Simba hata ikishinda michezo yake sita iliyosalia

Hata hivyo bado wana mchezo wa hatua ya robo fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United

"Mwezi huu tumekumbana na mechi ngumu kwenye ASFC tulihitaji kushinda ili kwenda nusu fainali, kwenye Ligi angalau tushinde nne kati ya sita ili tujihakikishie ubingwa lakini pia kuna robo ya Kombe la Shirikisho Afrika"

"Tunakutana na timu ngumu mfano Kagera Sugar ina wachezaji wazuri, mechi inayofuata ni Simba watani wetu wa jadi, hivyo tutatakiwa kupambana zaidi kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi,"anasema staa huyo wa zamani wa Coastal Union"

Mwamnyeto amesema kinachowasaidia kushinda ni uwepo wa makocha wazuri ambao wanawafanya wawe na utimamu wa mwili na akili

"Kocha Nabi ni mtaalamu wa kujenga akili za wachezaji kuamini kufanya mambo makubwa. Pia yupo kocha wa viungo ambaye anahakikisha muda wote tunakuwa fiti, hiyo pia kocha inampa nafasi ya kutumia wachezaji wote waliopo hivyo ni kazi kwetu kumuonyesha kwamba tunastahili kuaminiwa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’