Siku za karibuni kuna watu walianza kuzungumza sana kuhusu fundi Mburkinabe Stephane Aziz Ki
Leo Aziz Ki amewakumbusha wale walioanza kumbeza kuwa ni yuleyule, nyakati ngumu humkumba kila mchezaji
Mabao yake matatu leo yamemuongezea morali kuelekea mchezo wa dabi dhidi ya Simba siku ya Jumapili, April 16
Aziz Ki alihitaji mechi moja nzuri ili kurejesha 'confidence' yake na jambo jema ameipata mechi hiyo leo hivyo wale wanaofuata wajiandae
Aziz Ki amefikisha mabao nane msimu huu na assist nne. Sasa yuko tayari kwa majukumu makubwa zaidi!
Mbele kuna Fiston Mayele, Aziz Ki chini yake, kule pembeni kuna Bernard Morrison au Jesus Moloko, upande mwingine kuna Kennedy Musonda huku bwa mdogo Clement Mzize akisubiri dakika zake!
Tukutane April 16...!
ADVERTISE HERE