Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Angetile Osiah ameeleza kushangazwa na hatua iliyochukuliwa na mchezaji Feisal Salum kwenda TFF kuomba kuvunja mkataba wake na Yanga
Osiah amesema ni jambo linalofikirisha pale mchezaji anapoiomba taasisi nyingine ivunje mkataba wake katika klabu anayoitumikia, ni dalili mbaya kuwa mpira wetu unakwenda katika mwelekeo usiofaa
Osiah alitoa maoni yake kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii;
"Mpira wetu unaenda siko. Mchezaji ana mkataba na klabu, halafu anaiomba taasisi nyingine ivunje huo mkataba! Logic inakataa kabisa"
"Afadhali angetaja hayo manyanyaso, lakini inaonekana ni utashi tu wa kutaka kuondoka. Huu ni ubabaishaji"
"Mtu ambaye amechoshwa na ubabaishaji angeomba kuondoka na klabu ambayo inamtaka ingejitokeza kumalizana na muajiri wake"
"Football ina kanuni tofauti na ajira nyingine ambazo unaweza kuvunja mkataba wakati wowote unapopata greener pasture"
"Hivi akivunja mkataba ndio ataanza kutafuta klabu inayomfaa? Hizo ni sinema, Uaminifu na uadilifu wa mtu hupimwa katika mambo kama haya"
"Respect aliyoipata na vitu vinavyofanyika ni vitu viwili tofauti. Alishakuwa mchezaji mkubwa lakini anazidi kushusha hadhi yake. Kuaminika baadaye huko aendako itakuwa issue," aliandika Osiah