Msimu huu Wananchi wamekuwa na wakati mgumu inapokuja changamoto ya mikwaju ya penati
Sio kwamba Yanga haina wapiga penati wazuri la, lakini kilichotokea ni kukosa kujiamini kwa wachezaji hasa baada ya mfululizo wa kukosa mikwaju hiyo
Penati pekee ambayo Yanga walifunga kwenye ligi ni kupitia kwa Bernard Morrison katika mchezo wa mkondo wa kwanza ligi kuu dhidi ya Geita Gold
Lakini tangu majukumu ya kupiga mikwaju ya penati yaachwe kwa Stephane Aziz Ki, mambo yamekuwa tofauti
Aziz Ki ni kama amemaliza 'mkosi' wa kukosa penati kwa Yanga akifunga penati tatu mfululizo
Juzi katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar, Aziz Ki alifunga penati mbili na kuondoka na mpira baada ya kufunga 'hat-trik'
Kwa sasa Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amemkabidhi Aziz Ki majukumu ya kupiga penati na hata mipira ya adhabu ambayo wakati mwingine Kennedy Musonda na Djuma Shaban nao hupiga