Ligi Kuu ya NBC inaelekea ukingoni Yanga ikisalia na mechi tano kuhitimisha msimu huku ikiwa na nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wake kwa msimu wa pili mfululizo
Mshambuliaji Fiston Mayele anongoza orodha ya wafungaji akiweka kambani mabao 16, nae yuko kwenye nafasi nzuri ya kuibuka mfungaji bora
Mayele ameifikia rekodi yake ya msimu uliopita ambapo pia alifunga mabao 16 akizidiwa bao moja na George Mpole aliyekuwa akiitumikia Geita Gold ambaye alifunga mabao 17
Mayele anaweza kuvunja rekodi yake ya mabao akihitaji kufunga angalau bao moja kutoka katika mechi tano zilizobaki
Mlinda lango Djigui Diarra nae yuko katika nafasi ya kuvuka rekodi ya cleansheet 15 ambazo zilimpa tuzo ya kuwa kipa bora msimu uliopita
Tayari Diarra amefikisha cleansheet 15 nae akiwa na mechi tano kuvunje rekodi hiyo
Msimu uliopita Yanga ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ikiwa alama 74 baada ya mechi 30, wakifunga mabao 49 na kuruhusu mabao nane tu
Mpaka sasa Yanga imefikisha alama 68 baada ya mechi 25, ikifunga mabao 50 na kuruhusu mabao 11 kutikisa nyavu zake
Yanga inahitaji kushinda mechi mbili kati ya tano kufikia na hata kuvunja rekodi yake ya alama 74 za msimu uliopita