Pluijm ampa tuzo Mayele mapemaa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Apr 2023
Pluijm ampa tuzo Mayele mapemaa

Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Van Der Pluijm amesema licha ya kubakia michezo minne ili msimu kuisha ila kwake binafsi hadi sasa mchezaji bora ni mshambuliaji na kinara wa ufungaji bora Ligi Kuu Bara nyota wa Yanga, Fiston Mayele

Mayele alifunga bao moja katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Kagera Sugar na kumfanya nyota huyo kufikisha mabao 16 msimu huu akiifikia rekodi aliyoiweka msimu uliopita nyuma ya aliyekuwa mshambuliaji wa Geita Gold, George Mpole aliyefunga 17.

Pluijm amesema wapo wachezaji wengi ambao wamefanya vizuri ila Mayele ameonyesha utofauti mkubwa

"Kuona mchezaji anafunga mabao 15 na kuendelea kwa misimu miwili mfululizo sio jambo la kawaida na wengi wamekuwa hawana hicho kiwango. Ana spidi, anajua jinsi ya kujipanga, utulivu wake mbele ya lango la mpinzani na ni mmaliziaji mzuri" alisema Pluijm

Mholanzi huyo pia alisema kitu kingine kinachomtofautisha Mayele na wengine ni kutokuwa na majivuno kwani baadhi yao wakiona wamefanikiwa hujisahau jambo linalowafanya kuzorotesha vipaji vyao pindi tu wanapoyazoea mazingira ya sehemu husika.

Wakati Pluijm akiongea hayo ila Mayele ana kazi kubwa ya kufanya katika michezo mitano iliyobaki kwa Yanga kwani kati ya hiyo ni timu mbili tu ambazo hajazifunga ikiweno Simba anayoenda kukutana nayo Jumapili hii na mchezo wa mwisho dhidi ya Tanzania Prisons.

Katika michezo iliyobaki kwa Yanga mbali na hiyo ni dhidi ya Singida Big Stars ambao tayari mchezo wa kwanza ameifunga mabao matatu (Hat-Trick) huku Dodoma Jiji na Mbeya City kila mojawapo akiwa ameifunga mawili katika mzunguko wa kwanza.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’