Wananchiiii ile siku imewadia! Ni mchezo dhidi ya watani Simba ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kuzisaka alama zote tatu ili kujihakikishia ubingwa wa ligi kuu mapema
Wananchi wanataka kwenda Nigeria kuikabili Rivers United wakiwa tayari wamemaliza mbio za ubingwa hapa nyumbani
Chini ya Kocha Nasreddine Nabi, Yanga haijawahi kuwa na 'shoo mbovu' mbele ya watani zao Simba
Meneja wa Habari na Mawasiliano Ali Kamwe amesema leo ni kilele cha 'kuwakanda' Simba
Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga wajitokeze kwa wingi dimba la Mkapa katika mchezo huo ambao ushindi ndio matokeo yanayohitajika
Twendeni kwa wingi tukajihakikishie ubingwa wetu....!
ADVERTISE HERE