Uamuzi wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuwagomea Rivers United kutumia uwanja wao wa Adokiye Amiesimaka, Port Harcourt katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga unaweza kuwa na faida kwa Wananchi
Rivers United walitarajia kupata kibali kutoka kwa CAF, kurejea katika uwanja wao huo wa nyumbani baada ya ukarabati mkubwa kukamilika
Lakini maombi yao yalitupiliwa mbali na CAF na badala yake wataendelea kucheza michezo yao ya nyumbani kwenye Uwanja wa Godswill Akpabio unaobeba takribani mashabiki 10,000 tu wakati dimba lao la Adokiye Amiesimaka linachukua hadi mashabiki 40,000
Rivers United walicheza mechi za hatua ya makundi katika uwanja wa Godswill Akpabio wakishinda mechi mbili na kutoka sare mchezo mmoja. Ni wazi wana hofu ya kutumia uwanja wa Godswill Akpabio kutokana na kutokuwa na mashabiki wao wengi
Mtanange wa Jumapili dhidi ya Yanga utachezeshwa na mwamuzi wa Afrika Kusini Abongile Tom
Mchezo huo ni kama utakuwa ukichezwa katika uwanja 'neutral' na Yanga inayo nafasi ya kupata matokeo mazuri katika mchezo huo
Yanga inahitaji kusaka ushindi ugenini na pale itakaposhindikana hata matokeo ya sare yatakuwa mazuri