Kikosi cha Yanga kitaondoka nchini Alhamisi Alfajiri kupitia shirika la ndege Ethiopia kuelekea Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya kombe la Shirikisho la CAF barani Afrika dhidi ya Rivers United. Mchezo huo utapigwa Jumapili April 23 katika Mji wa Uyo
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema timu itawasilia Lagos saa 6 mchana siku hiyohiyo ya Alhamisi na wataweka kambi ya siku moja, wataondoka Lagos siku ya Ijumaa kuelekea Mji wa Uyo ambao mchezo utapigwa
"Tutaondoka na msafara wa watu 49 ukijumuisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, taarifa zaidi itatolewa kupitia platform zetu za kidigitali"
"Yanga itakuwa na siku mbili za mazoezi katika Mji wa Uyo kuelekea mchezo utakaopigwa Jumapili, April 23 saa 10 jioni kwa saa za Tanzania"
"Wachezaji wote wako hatika hali nzuri, hakuna mchezaji aliyepata majeraha baada ya mechi dhidi ya Simba. Yanga ilirejea kambini jana na leo watakamilisha maandalizi ya mwisho Avic Town kabla ya safari," alisema Kamwe
Kamwe amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga kuiombea timu yao kwa kila namna inayofaa ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri huko Nigeria
"Hii ni nafasi adimu ya kwenda hatua ya nusu fainali, Wanayanga tuungane kuhakikisha tunafanikisha lengo letu. Hatua hii tuliyofika ni ngumu hivyo tunapaswa kuungana kuipa sapoti timu yetu. Tuiombee timu yetu kwa namna inayofaa ili tupate matokeo mazuri ugenini"