Beki wa Yanga Mamadou Doumbia ambaye alisafiri Mali kuhudhuria msiba wa Baba yake, atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachosafiri Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema msafara wa Yanga utaondoka nchini Alfajiri ya Alhamisi, April 20 wakitumia usafiri wa ndege ya Ethiopia Airline
Kamwe amesema Doumbia ataungana na timu Ethiopia ambako wataunganisha ndege kuelekea Lagos, Nigeria
"Doumbia alikwenda Mali kuhudhuria mazishi ya Baba yake Mzazi, tunashukuru alipata nafasi ya kumpumzisha Mzee wetu salama na ataungana nasi Ethiopia ambako tutaunganisha ndege kwenda Lagos, Nigeria" alisema Kamwe
ADVERTISE HERE