Mchezo wa ligi kuu kati ya Singida BS dhidi ya Yanga ambao uliahirishwa kutokana na ushiriki wa Yanga kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC), sasa utapigwa May 03 katika uwanja Liti, Singida
Wananchi watalazimika kuweka kambi huko Singida kwani baada ya mchezo huo, siku tatu baadae watarudi tena uwanja wa LITI kuumana na Singida BS katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambao utapigwa May 07
Zitakuwa dakika 180 za mapambano kwa Yanga ikihitaji kushinda mechi zote mbili
Yanga inahitaji kutetea ubingwa wa ligi kuu, ushindi dhidi ya Singida BS utawasogeza karibu zaidi kufikia malengo kwani wanahitaji alama nane kutoka mechi nne zilizobaki
Ili kutetea kombe la FA Yanga lazima ishinde dhidi ya Singida BS kutinga fainali zaidi Wananchi wanaomba watani zao Simba washinde dhidi ya Azam Fc ili 'kipigwe' tena derby katika FA