Kwa mujibu wa mtandao wa FotMob, klabu ya Yanga imeongoza katika klabu zilizofanya vizuri hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa kutoka mechi zote sita za hatua ya makundi
Timu zilizoifuatia Yanga ni FAR Rabat, US Monastir, Pyramids na Asec Mimosas
Yanga ilimaliza kileleni mwa kundi D ikikusanya alama 13 baada ya mechi sita
Wananchi walishinda mechi nne, kutoka sare moja na kupoteza moja
Yanga tayari imewasili Nigeria kuikabili Rivers United kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya michuano hiyo

ADVERTISE HERE