Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji wana nafasi ya kuandika historia kwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya Rivers United ambao utapigwa leo huko Nigeria
Kamwe amesema ni mechi ngumu inayotarajiwa kuwa na ushindani lakini hizo ndio mechi ambazo hujenga majina ya wachezaji na kuwapa heshima
"Hizi ndio aina ya mechi wachezaji wakubwa huzihitaji kwenye career zao! Mechi zilizobeba Historia ya Klabu. Ni nafasi ya kipekee kwa wachezaji wetu kuyaandika majina yao kwa wino wa dhahabu kwenye vitabu vya historia ya Yanga"
"Tuliweza Tunisia, Tuliweza Mali, Tukaweza Lubumbashi, sioni ioni sababu ya kushindwa hapa Nigeria. Haitakuwa mechi rahisi ya nyumbani kama Hatutavuja jasho ugenini"
"Hizi za leo ndio dakika 90 za maamuzi. Nimewaona siku mbili mazoezini, nimeona utayari wenu katika mpambano wa leo. Tuwe mchezoni kutoka sekunde ya kwanza hadi ya mwisho. IN SHAA ALLA INAWEZEKANA. Twendeni Tukaipambanie YANGA. Twendeni Tukawape Furaha Wanayostahili WANANCHI"