Yanga ndio klabu pekee iliyopata ushindi ugenini katika mechi za mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho la CAF baada ya kuichapa Rivers United mabao 2-0
Pyramids Fc wakiwa kwao Misri wakalazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Malumo Galants kutoka Afrika Kusini
Kama Yanga itafanikiwa kutinga nusu fainali, itakutana na mshindi wa jumla wa mchezo kati ya Galants dhidi ya Pyramids ambao utapigwa Jumapili ijayo huko Afrika Kusini
US Monastir wakiwa kwao Tunisia, wamelazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Asec Mimosas wakati US Alger wakishinda mabao 2-0 dhidi ya AS FAR
Mechi za mkondo wa pili zitapigwa April 30, zitaamua timu nne zitakazofuzu nusu fainali
ADVERTISE HERE