Bonasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan inaendelea, jana Milioni 10 ilisoma kwenye akaunti ya Yanga baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United huko Nigeria
Tangu hatua ya makundi, Yanga imepachika jumla ya mabao 10 na hivyo sasa imepata bonasi ya Tsh Milioni 50 kutoka kwa Mama
Bado mechi ya marudiano dhidi ya Rivers United ambayo itapigwa Jumapili, April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Wananchi wana nafasi ya kuongeza 'mkwanja' katika akaunti yao
Pongezi kwa wachezaji, benchi la ufundi, Rais Injinia Hersi Said pamoja na viongozi wenzake kwa kuhakikisha Wananchi wanaendelea kuwa na furaha
ADVERTISE HERE