Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema njia pekee itakayoziwezesha timu za Tanzania kufanikiwa kwenye michuano ya Kimataifa ni kufanya uwekezaji.
Dk Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa jana, aliyazungumza hayo muda mfupi baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers ambapo wenyeji walichapwa mabao 2-1.
Dk Mwakyembe amesema klabu ya Township Rollers inaonekana kukamilika na ina wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa ukifananisha na wale wa kikosi cha Yanga.
Amesema Yanga inahitaji kufanya mabadiliko ya mfumo wake ili kuleta wawekezaji watakaofanikisha 'kifedha' kutengeneza kikosi imara na cha ushindani zaidi.
Dk Mwakyembe aliipongeza klabu ya Simba ambayo tayari imekamilisha mchakato huo wa kupata mwekezaji sasa ikiwa inakamilisha mambo ya kiofisi tayari kwa mwekezaji mpya kukabidhiwa timu.
Yanga nayo tayari imeanza hatua za awali kubadilisha mfumo wake wa uendeshaji kwendana na hali halisi ya wakati huu.
Tayari Kamati iliyokuwa imeundwa kupendekeza mfumo sahihi wa uendeshaji imekamilisha kazi na kinachosubiriwa ni kuitishwa kwa Mkutano Mkuu utakaopitisha/kukataa mapendekezo hayo.

ADVERTISE HERE