Yaliyo nyuma ya pazia kikosini Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
8 Mar 2018
Yaliyo nyuma ya pazia kikosini Yanga
Kulingana na mtandao wa Bin Zubeiry Sports Online, bado swala la ulipaji mishahara ya wachezaji limeendelea kuutesa uongozi wa Yanga baada ya kubainika sasa ni miezi minne wachezaji hawajalipwa mishahara yao.

Imeelezwa hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa morali ya wachezaji kushuka na ndiyo maana wengi wao wanaonekana kucheza chini ya viwango vyao kwa sasa.

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kwamba suala la mishahara ni siri baina ya mwajiri na mwajiriwa.

“Mishahara ya mchezaji na ofisi ni vitu binafsi, siwezi nikavisemea hivyo. Sisi siyo taasisi peke yake ambayo haijalipa watu mishahara, taasisi zipo nyingi mpaka wakati mwingine serikalini,”alisema.

Mkwasa amesema hata Waandishi wa Habari pia kwenye vyombo mbalimbali vya Habari nao hawajalipwa zaidi ya miezi sita na Habari haziandikwi, akasistiza masuala ya klabu na waajiri wake yaachwe kuwa siri.

Hali ni mbaya ndani ya Yanga kwa ujumla, kwani hata benchi la Ufundi pia, kuanzia Kocha Mkuu George Lwandamina na Wasaidizi wake wote, Mzambia mwenzake Noel Mwandila, wazawa Nsajigwa Shadrack, Juma Pondamali kocha wa makipa, Mohammed Omar ‘Mpogolo’ mtunza vifaa, Jacob Onyango mchua misuli, Meneja Hafidh Saleh na Daktari Edward Bavu nao hawajalipwa kwa zaidi ya nusu mwaka.

“Hapa maisha ni magumu mno, na mbaya zaidi viongozi kabisa wale wa timu sijui Mwenyekiti (Clement Sanga) na wasaidizi wake hatuwaoni. Sana tunakuwa na Nyika. Wale tunawaolalamikia (Sekretarieti na Makocha) wao nao hali ndiyo mbaya zaidi,” amesema mmoja wa wachezaji, jina tunalifadhi.

“Yaani watu hapa wanaenda kwa kudra za Mungu tu, kila mtu akili yake haipo kabisa kazini, hakuna morali kabisa. Ni kocha tu ajaribu kutumia busara zake angalau tunaingia uwanjani kucheza,”ameongeza.

Tangu kuondoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji, changamoto ya ulipaji mishahara ya wachezaji imekuwa kubwa sasa hali hiyo inaiweka Yanga kwenye wakati mgumu msimu huu.

Nadhani ni wakati muafaka kwa wanachama na mashabiki wa Yanga kuutaka uongozi uharakishe zoezi la mabadiliko ili kuinusu timu isije ikaumbuka zaidi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →