Ni Jumapili hii pale uwanja wa Benjamin Mkapa, Wananchi watakuwa na jambo la Kitaifa
Ni katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United
Yanga ikiwa mbele kwa mabao 2-0 ushindi waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Nigeria, ushindi au matokeo yoyote ya sare siku ya Jumapili yataipeleka Yanga nusu fainali
Itakuwa Jumapili ya kivumbi na jasho! Yanga ikiwania rekodi ya kutinga nusu fainali ya kihistoria
Hii sio mechi ya kukosa! Nunua tiketi yako mapema ili kuhakikisha unakuwa sehemu ya mafanikio haya
NI JUMAPILI YA KIVUMBI NA JASHO...!
ADVERTISE HERE