Twendeni tukajaze Benjamin Mkapa - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Apr 2023
Twendeni tukajaze Benjamin Mkapa - Kamwe

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema ni nafasi adimu kwa mashabiki wa Yanga nchini kushuhudia timu yao ikitinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Kamwe amesema Wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United

Kamwe amesema pamoja na ushindi wa mabao 2-0 waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza, lakini bado hawajafikia malengo, wachezaji wao wanahitaji sapoti ya mashabiki kuhakikisha wanaibuka na ushindi na kufuzu nusu fainali

"Yanga tunajivunia matokeo ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United ugenini lakini tunajua bado tuna kazi ya kufanya tuweze kutinga nusu fainali"

Tunataka mashabiki waujaze uwanja wa Benjamin Mkapa katika Jumapili ya Kivumbi na Jasho itakayokuwa ya kihistoria kwa Yanga kufuzu nusu fainali. Tunataka mpaka kufikia siku ya Jumamosi tiketi zote kuelekea mchezo ziwe zimemalizika"

"Mashabiki wote watakaokuja uwanjani Jumapili wahakikishe wamevaa jezi au mavazi ya njano na kijani, tunataka uwanja wote uwe njano na kijani," alisema Kamwe

Kamwe amesema hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Rivers itazinduliwa siku ya Ijumaa, mchana Tandika jijini Dar es salaam

Ijumaa asubuhi kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu litakalofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam

Siku ya Jumamosi kutakuwa magari matano ambayo yatakuwa yakiuza tiketi maeneno mbalimbali ndani ya jiji la Dar es salaam

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
59m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’