Bacca ataja siri ya ubora wake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Apr 2023
Bacca ataja siri ya ubora wake

Mlinzi wa kati ya Yanga Ibrahim Bacca amefichua siri ya kuimarika kwa kiwango chake katika msimu mmoja ambao amewatumikia mabingwa hao wa Tanzania

Tangu ajiunge na Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu uliopita akitokea klabu ya KMKM, Bacca ameshuhudiwa kiwango chake kikiimarika na sasa akifanikiwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza cha Kocha Nasreddine Nabi pia akiitwa kwa mara ya kwanza na kucheza kwenye timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

Bacca amesema ubora wa wachezaji anaocheza nao kwenye safu ya ulinzi ndio siri ya mafanikio yake akieleza kujifunza na kupata ushirikiano kutoka kwao

Yanga inayoundwa na ukuta wa Joyce Lomalisa, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Bacca, Mamadou Doumbia, Djuma Shaban, Kibwana Shomari na Yanick Bangala

Bacca amesema anafurahi kucheza na mabeki wote waliopo Yanga kutokana na kila mmoja kuwa na aina yake ya uchezaji

"Mabeki wote nimepata nafasi ya kucheza nao wana uwezo na ni viongozi wazuri kiwanjani lakini nafurahi zaidi nikicheza na beki mwingine kati na Bangala akawa juu kama namba sita ni mtu makini sana na anapenda kuzungumza mimi namuita beki kiongozi"

"Mkicheza uwanjani kwa kukumbushana majukumu mchezo wa mpira ni mwepesi na makosa mengi yanapungua tuna nahodha Mwamnyeto anazungumza ana kila sifa ya kuwa kiongozi lakini kuna Bangala hapendi timu ifungwe kizembe"

"Siwezi kutaja sifa za kila mchezaji ila kile kinachoonekana uwanjani kinatokana na kuaminiana na kupeana maelekezo ili kila mmoja aweze kufanya kwa ubora na timu ipate matokeo mazuri," alisema Bacca

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’