Klabu ya Yanga leo inazindua rasmi hamasa na shamrashamra kuelekea mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United
Ni tukio kubwa la aina yake litakalofanyika saa nane mchana Temeke, Mwembe Yanga ambapo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na Mzee wa Bwax na Sir Jay
Katika tukio hilo Wananchi watapata burudani, kununua tiketi, jezi na kuweka mikakati ya ushindi siku ya Jumapili
Ni kuelekea Jumapili ya Kivumbi na Jasho pale uwanja wa Benjamin Mkapa! Jumapili ya kuisaka nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika kwa mara ya kwanza

ADVERTISE HERE