Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mh Kassim Majaliwa amechangia tiketi 1000 kuwawezesha Wananchi kushuhudia mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Rivers United
Mchezo huo utapigwa Jumapili April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 1 usiku
Tiketi hizi ni maalum kwa mashujaa wanaojitokeza kwenye zoezi la uchangiaji damu
Klabu ya Yanga imeyakaribisha Makampuni/Taasisi mengine kununua tiketi kwa ajili ya kuwazawadia mashujaa wote wanaojitolea damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wengine

ADVERTISE HERE