Baada ya kufanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United, Yanga itachuana na Malumo Galants ya Afrika Kusini katika hatua ya nusu fainali
Mchezo wa kwanza utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, May 10 na mechi ya pili kupigwa May 17 huko Afrika Kusini
Malumo wametinga nusu fainali baada ya kuiondosha Pyramids kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1
Leo wameshinda bao 1-0 huko Afrika Kusini wakati mchezo wa kwanza uliopigwa Misri ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Hii ni nafasi nyingine kwa Yanga kutinga fainali....!
ADVERTISE HERE