Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga Yusufu Manji alikuwepo uwanja wa Benjamin Mkapa jana kushuhudia timu yake ikiandika historia ya kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Manji alikuwa chachu ya mafanikio ya Yanga kati ya mwaka 2010 na 2016 akiwa Mdhamini/Mfadhili
Yanga ilicheza makundi ya kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza msimu wa 2015/16, wakati huo Manji akiwa ndio Mwenyekiti
Wengi wanaamini kama sio changamoto zilizomkumba mwaka 2016, pengine Wananchi wangeyafikia mafanikio haya zamani
Bado Manji ni Mwananchi kindakindaki na jana amedhihirisha kwa kuungana na Wananchi wenzake kufurahia mafanikio baada ya Yanga kutinga nusu fainali ya Shirikisho
ADVERTISE HERE