Kikosi cha Yanga kiko mkoani Singida kukamilisha mchezo wa kiporo ligi kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars ambao utapigwa kesho Alhamisi, May 04 katika uwanja wa LITI
Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga ili kushinda ili kuzidi kusogea karibu na ubingwa wa 29
Baada ya mchezo huo Yanga itarejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Malumo Galants
Mchezo huo utapigwa Jumatano ijayo May 10 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Benchi la ufundi la Yanga tayari limeanza mkakati wa kuhakikisha Yanga inakata tiketi ya kutinga fainali ya michuano hiyo
Yanga imeanza kukusanya taarifa za Marumo ambayo kwenye ligi kuu ya Afrika Kusini inashika nafasi ya 14 kati ya timu 16
Hata hivyo Malumo wamekuwa na mwenendo mzuri kwenye michuano ya Shirikisho na haishangazi kwani ni kawaida kwa timu za Afrika Kusini kutofanya vizuri kwenye ligi ya ndani lakini kufanya vizuri Kimataifa
Kaizer Chiefs imewahi kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika misimu miwili nyuma wakati kwenye ligi ikiwa nafasi ya 9
Ilikuwa hivyo kwa Orlando Pirates msimu uliopita wakicheza fainali ya Shirikisho wakati kwenye ligi wakimaliza katika nafasi ya 5
"Niliwaona mechi yao moja ya hatua ya makundi sio timu rahisi tunatakiwa kujipanga sawasawa, tayari tumeshaanza kutafuta taarifa zao zaidi lakini niseme tunatakiwa kuiheshimu kwa kufika kwao nusu fainali, zitakuwa ni mechi mbili ngumu za nusu fainali,"alisema Nabi
"Najivunia kikosi changu, naamini wanatambua kwamba kama watajiongeza kidogo kuna rekodi kubwa tunaweza kuiweka msimu huu lakini haitakuja kirahisi tunatakiwa kuvuija jasho zaidi ya kote tulikotoka"