Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wanatarajia mchezo wenye ushindani kutoka kwa Singida BS katika ligi kuu ya NBC hapo kesho
Kaze amesema wanahitaji kuhamisha ubora walioonyesha kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la CAF (CAF CC) katika mchezo huo utakaopigwa uwanja wa LITI
"Tunajua rekodi nzuri ya Singida BS kwenye uwanja wao. Ni timu iliyojiimarisha ikiwa katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi na pia ni timu yenye wachezaji wazoefu wa ligi"
"Lakini ili tufikie malengo yetu tunapaswa kutafuta matokeo mazuri kwenye mchezo huo kwa hiyo tumejiandaa kuwa na mchezo mzuri ili kutafuta alama tatu ambazo zitatusogeza karibu na ubingwa msimu huu," alisema Kaze
Akizungumzia hali ya kikosi, Kaze amesema mchezaji Yannick Bangala atakosekana katika mchezo huo akiwa ni majeruhi huku wachezaji Salum Abubakar 'Sure Boy' na Fiston Mayele wakipata changamoto ndogo za kiafya
Kaze amesema wachezaji hao watashiriki mazoezi ya mwisho leo na watajiridhisha na utimamu wao lakini amesisitiza Yanga imedhihirisha kuwa na kikosi imara, mchezaji mmoja anapokosekana yule anayepewa nafasi atafanya vizuri