Picha linaanza, kabla ya mechi ya ligi kuu kati ya Singida BS dhidi ya Yanga kupigwa pale uwanja wa Namfua LITI jioni ya leo, kiungo fundi wa Singida BS Bruno Gomez anakwenda kusalimiana na Kocha Nasreddine Nabi na pia kusalimiana na wachezaji na maafisa wa Yanga waliokuwa katika benchi
Mchezo unamalizika baada ya dakika 90, Yanga inaibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kujiweka karibu kabisa na ubingwa wa 29
Baada ya mchezo kiungo fundi wa Yanga Stephane Aziz Ki anakutana uso kwa uso na Bruno na wawili hao kuwa na mazungumzo ya muda mfupi huku kocha wa makipa Nienov akifanya kazi ya kutafsiri kile alichokuwa akizungumza Aziz kwa Bruno
Yalikuwa mazungumzo ya kutakiana heri na kupongezana baada ya kazi kubwa wakati msimu ukimalizika kuelekea msimu ujao
Mafundi hao wa mpira wana mambo yanayofanana, wote wamefunga mabao tisa kwenye ligi kuu msimu huu na wote ni mafundi kwelikweli wa kupiga mipira iliyokufa! Wote si walimtungua yule kipa kwa majirani bwana!
Wakati wawili hao wakiagana unakuja kukumbuka ile jezi namba sita pale Jangwani si haina mtu!