Yanga imeanza kunufaika na Kocha Cedric Kaze katika maendeleo ya soka la Vijana
Kaze aliteuliwa kuwa Mkiurugenzi wa Maendeleo ya soka la Vijana akichukua nafasi ya Mwinyi Zahera ambaye Mkataba wake ulimalizika mwezi Septemba 2022
Kaze ana CV kubwa katika soka la Vijana, kabla ya Yanga kumrejesha Afrika, alikuwa akifundisha kwenye moja ya Academy za FC Barcelona huko Canada
Kazi yake imeanza kuonekana Jangwani baada ya timu yake ya Yanga U17 kuanza kuonyesha makali kwenye ligi ya vijana umri wa chini ya miaka 17
Katika mechi mbili ambazo Yanga U17 wamecheza kwenye ligi hiyo, wameshinda zote huku wakifunga mabao 12 ushindi mabao 6-0 katika kila mchezo
Pamoja na kuendelea na majukumu yake ya Kocha Msaidizi wa Yanga, Kaze anapenda soka la vijana na mara kadhaa amefanya kazi ya kuwanoa vijana yeye mwenyewe
Chini ya Kaze, Wananchi watarajie kuwaona kina Clement Mzize wengi wakiibuliwa kutoka timu za vijana