Nabi akimtaka Bruno anatua

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 May 2023
Nabi akimtaka Bruno anatua

Yanga itamsajili kiungo mshambuliaji wa Singida BS Bruno Gomez kama kocha mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi atamuhitaji, imefahamika

Juzi baada ya mchezo dhidi ya Singida BS uliopigwa uwanja wa LITI na Yanga kushinda mabao 2-0, Bruno aliibua maswali miongoni mwa Wananchi baada ya kuonekana kwenye benchi la Yanga kabla ya mchezo akisalimiana na Nabi na wengine wote waliokuwa katika benchi

Baada ya dakika 90 za mchezo kukamilika, Bruno alionekana akizungumza na kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki 

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imedokeza kuwa hatma ya Bruno iko mikononi mwa Kocha Nabi ambaye atawasilisha mapendekezo yake baada ya msimu kumalizika

Yanga haitarajiwi kufanya usajili mkubwa katika dirisha lijalo la usajili, itasajili wachezaji wachache bora kwa ajili ya kuimarisha maeneo yenye changamoto

Eneo la kiungo wa ushambuliaji linaweza kuwa moja ya maeneo hayo ili kumuongezea ushindani Aziz Ki

"Suala la Gomez sio suala gumu ni uamuzi wa kocha tu (Nabi) akisema basi atatua Jangwani, hilo hata yeye Nabi anajua, tumemuachia atuambie kiufundi kama anamfaa au vinginevyo," kiongozi mmoja mwandamizi wa Yanga alinukuliwa na Mwanaspoti

Bruno ndiye kinara wa mabao kwenye kikosi cha Singida BS akifunga mabao tisa na kutoa pasi nne za mabao katika ligi kuu ya NBC msimu huu

Anaweza kutumika kama mchezaji kiraka kwani anamudu kucheza katika nafasi zote eneo la kiungo

Mwanzoni mwa msimu Kocha wa Singida BS Hans van Pluijm alimtumia kama kiungo mkabaji (namba 6) baadae akamsogeza namba 8 na sasa anamtumia kama namba 10 eneo ambalo ameonekana kulimudu zaidi akifunga mabao mengi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’