Hatutawadharau Marumo Gallants - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 May 2023
Hatutawadharau Marumo Gallants - Kaze

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema hawana hofu yoyote kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants

Yanga na Marumo zitachuana katika mchezo wa kwanza kesho Jumatano ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Yanga ikihitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga fainali ya michuano hiyo

Kaze amesema wamepata muda mzuri wa kujiandaa na mchezo huo huku pia wakipata nafasi ya kuwasoma wapinzani wao hao kuelekea mchezo huo

Kaze amebainisha kuwa wanatambua ubora wa wapinzani wao pamoja udhaifu wao na wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa kwanza nyumbani

"Tumepata muda wa kuangalia mechi yao na walipoteza, hii imetusaidia kupunguza presha, lakini tumeweza kuona mapungufu yao yapo katika nafasi zipi ambazo zinaweza kutusaidia kupata ushindi," alisema Kaze.

"Ukweli Marumo siyo wabaya na hatupaswi kuwadharau kutokana na nafasi waliyopo kwenye ligi ya kwao, kwa sababu ligi haina mtoano kama hii michuano ya CAF"

"Kikubwa tunaenda kucheza nao tukiwa hatuna presha kwa sababu tunajua tunaenda kucheza na mpinzani wa aina gani na yupo katika wakati gani, lakini tunachoweza kukiangalia upande wetu ni kutafuta matokeo ya ushindi," alisema Kaze

Marumo waliwasili nchini Alfajiri ya leo Jumanne kuelekea mchezo huo wa kwanza katika kusaka tiketi ya kutinga fainali ya michuano ya Shirikisho ya CAF

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’