Jana mechi mbili za mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika zilipigwa ambao Yanga ilikuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kupepetana na Marumo Gallants wakati ASEC Mimosas nao wakiwa nyumbani kupepetana na USM Alger
Yanga ndio timu pekee iliyobuka na ushindi, ASEC Mimosas walilazimishwa suluhu ya bila kufungana
Katika kikosi bora cha wiki Yanga iliyoshinda mabao 2-0, imetoa wachezaji saba
Djigui Diarra, Dickson Job, Ibrahim Hamad 'Bacca' na Mudathir Yahya wamejumuishwa katika kikosi hicho
Pia wamo Fiston Mayele na waliofunga mabao ya Yanga Stephane Aziz Ki na Bernard Morrison

ADVERTISE HERE