Kesho Jumamosi, May 13 Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Yanga inahitaji alama tatu tu ili kutwaa ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo, ukiwa ubingwa wa 29
Ushindi kwa Wananchi katika mchezo huo utawahakikishia kutimiza malengo mapema kabla ya safari ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya Marumo Gallants
Ni wazi Yanga itahitaji kufunga hesabu za ligi kuu mapema kwa kutangaza ubingwa hapo kesho
ADVERTISE HERE