Tunakwenda kupambana Afrika Kusini - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 May 2023
Tunakwenda kupambana Afrika Kusini - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema timu imeondoka Tanzania kuelekea Afrika Kusini ikiwa na lengo moja tu, kupata matokeo mazuri ambayo yatawavusha kwenda fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Jumatano, May 17 Yanga itashuka uwanja wa Royal Bafokeng kumenyana na Marumo Gallants katika mchezo ambao Yanga inahitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare ili kutinga fainali

"Tunakwenda Afrika Kusini kupambana. Tumepata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza, hili ni jambo jema kwetu hivyo tunajua nini tunapaswa kufanya katika mchezo wa pili"

"Kwa bahati nzuri katika mashindano haya timu yetu imekuwa na rekodi ya kufanya vizuri ugenini. Tunawaheshimu Marumo ni timu nzuri, ina wachezaji wazuri wanocheza soka la kuvutia lakini hata sisi tuna uzuri wetu unaotufanya tuweze kupata matokeo mazuri sehemu yoyote"

"Tumejipanga, tunaamini walimu waliiona vizuri Marumo Gallants katika mchezo uliopita hivyo watakuja na mipango ambayo itatuwezesha kupata ushindi na kuvuka hatua hii ya nusu fainali," alisema Arafat

Yanga imesafiri Alfajiri ya leo Jumapili ikiwa na msafara wa takribani watu 100 uliojumuisha wachezaji viongozi na mashabiki ambao miongoni mwao 55 wamegharamiwa na Serikali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
21h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’