Marumo ni wabishi kwao lakini Yanga iko tayari

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2023
Marumo ni wabishi kwao lakini Yanga iko tayari

Jumatano, May 17 Yanga itashuka uwanja wa Royal Bafokeng kumenyana na Marumo Gallants katika mchezo ambao Yanga inahitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare ili kutinga fainali

Kikosi cha Yanga kilitua Afrika Kusini jana na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa Watanzania waishio Afrika Kusini wakiongozwa na ubalozi wa Tanzania nchini humo

Baadae Yanga ilielekea Mji wa Rustenburg ulio umbali wa takribani kilomita 133 kutoka Johannesburg

Mchezo dhidi ya Marumo Gallants utapigwa katika Mji huo majira ya saa 1 usiku kwa saa za Tanzania siku ya Jumatano

Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi kwa kuangalia takwimu za Marumo wanapokuwa katika uwanja wao wa nyumbani

Katika mechi za kombe la Shirikisho msimu huu kuanzia hatua ya mtoano na makundi, Marumo wameshinda mechi zote walizocheza nyumbani

Wakati Yanga ikiondoka uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jana, Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Nasreddine Nabi alisema wanakwenda kucheza mechi ngumu ambayo itawahitaji wachezaji wake kuwa makini na kuvuja jasho jingi ili kupata matokeo mazuri

Yanga iko mbele kwa mabao mawili kutokana na ushindi wa 2-0 waliopata katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam, ushindi, sare na hata kupoteza kwa tofauti ambayo sio zaidi ya bao moja, yatakuwa matokeo ambayo yataipeleka Yanga fainali

Nyota wa Yanga wako tayari kupambana ili kuhakikisha wanakwenda fainali. Mafanikio ya aina hii hayatokei kila mwaka, rekodi zimeandikwa na zinaweza kudumu kwa miaka mingi kwa kizazi hiki cha wachezaji wa Yanga

Msimu huu katika mashindano yote ya CAF (Ligi ya Mabingwa na Shirikisho) Nabi amepoteza mechi mbili tu ugenini dhidi ya Al Hilal na US Monastir

Wananchi wanamuamini na bila shaka ataandaa mkakati wa kukabiliana na Marumo huko kwao na kuhakikisha Yanga inapata matokeo mazuri ugenini na kufuzu hatua ya fainali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’