Yanga imejichimbia katika Hoteli ya The Royal Marang katika Mji wa Rustenburg Afrika Kusini ikiendelea na maandalizi ya mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants
Hoteli hii ina historia ya kipekee kwani ndipo ilipokuwa kambi ya timu ya Taifa ya Uingereza wakati wa michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika Afrika Kusini mwaka 2010
Ndani ya eneo la Hoteli hiyo kuna uwanja wa mazoezi ambao ulitengenezwa na Waingereza kwa ajili ya timu yao kuutumia katika maandalizi kwenye kombe la Dunia 2010
Ni katika uwanja huo Yanga inafanya maandalizi yake kwa ajili ya kuwakabili Marumo Gallants hapo kesho




ADVERTISE HERE