Rais wa Yanga Injinia Hersi Said jana alifanya mahojiano na Mwanahabari maarufu Afrika Kusini Robert Marawa kupitia redio 947
Hersi alizungumzia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na malengo ya klabu ya Yanga kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kesho Wananchi wakikamilisha mchezo wa pili wa nusu fainali dhidi ya Marumo Gallants lengo likiwa kutinga fainali
Hersi pia alizungumzia mipango mikubwa zaidi ya msimu ujao ikiwemo maboresho ya kikosi yanayotarajia kufanyika ili kuhakikisha Yanga inaendelea kufanya vizuri katika mashndano yote msimu ujao
Hersi alibainisha kuwa kuna mchezaji mwenye 'profile' kubwa kutoka Ligi ya Afrika Kusini wako katika mpango wa kumsajili
"Msimu ujao tumepanga kusajili mchezaji mmoja kutoka Ligi Kuu ya Afrika Kusini. Yupo mchezaji ametuvutia sana, tumepanga kumleta Ligi ya Tanzania," alisema Hersi
Hata hivyo pamoja na maswali ya udadisi kutoka kwa Marawa, Hersi hakuwa tayari kumtaja mchezaji huyo wana timu anayocheza
"Hatuwezi kuweka kila kitu wazi sasa kwa sababu tunajua bado ana mkataba na timu yake lakini itakuwa suprise hapa Afrika Kusini," aliongeza Hersi
Yanga inahusishwa na wachezaji wawili kuroka Afrika Kusini, kiungo mshambuliaji Khanyisa Mayo anayecheza Cape Town City na Ranga Chivaviro wa Marumo Gallants
Mayo anaongoza orodha ya wafungaji bora wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini akifunga mabao 12 sawa na Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns
Za ndaani kabisa ni kuwa, jicho la Yanga limetua kwa Mayo, huyu ndiye ambaye Wananchi wanaweza kumshuhudia akiwa na uzi wa njano, kijani na nyeusi msimu ujao