Hatma ya fainali iko mikononi mwetu - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 May 2023
Hatma ya fainali iko mikononi mwetu - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wana dakika 90 ngumu za kuipigania heshima ya Yanga katika mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants

Yanga tayari iko Afrika Kusini ikijiandaa na mchezo huo ambao utapigwa kesho Jumatano, saa 1 usiku. Yanga iko mbele kwa mabao 2-0 ushindi waliopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Hata hivyo Nabi amesema mchezo wa kesho ni tofauti, hawafikirii matokeo ya mchezo wa kwanza, watahitaji kupambana ili kupata matokeo mazuri yatakayowavusha hatua ya fainali

"Tunakwenda kwenye mchezo utakaoamua hatma yetu kama tutamalizia mguu wa pili kwenda fainali au vinginevyo, mimi ukiniuliza nitarudia kukwambia hii ni mechi ngumu kwetu kuliko ile ya kwanza"

"Nimewaambia wachezaji wangu kwamba tunatakiwa kuipigania heshima ya klabu yetu kwa kucheza kama wanajeshi, tuna jukumu la kuipigania Yanga na Tanzania"

"Natamani kuona kila mchezaji akicheza kwa jihadi na kujitolea nguvu zake zote kama anavyocheza beki wetu Bacca, napenda sana kumuona anavyojituma uwanjani, tunatakiwa kukaba kwa nguvu na kushambulia kwa nguvu lakini kikubwa tukipata nafasi tuzitumie"

"Wapinzani wetu watakuja na nguvu kubwa kutokana na matokeo ya mchezo uliopita nasi tunatakiwa kuwa na nguvu ya kutoruhusu watufunge kuwathibitishia kwamba hatukubahatisha," alisema Nabi

Leo Yanga itakamilisha mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Royal Bafokeng ambao utatumika katika mchezo siku ya Jumatano

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’